Kenya yabadilisha kauli kuhusu mazungumzo yake na China
2 Aprili 2025Matangazo
Katika chapisho hilo la leo asubuhi kwenye mtandao wa X, wizara ya fedha ya Kenya, ilisema kuwa waziri huyo wa China alielezea kujitolea kusimamia mazungumzo kuhusu urekebishaji wa madeni na ufadhili wa masharti nafuu kusaidia uthabiti wa kiuchumi wa Kenya.
Tarifa yachapishwa upya bila maelezo zaidi
Taarifa hiyo ilifutwa baadaye na kuchapishwa tena bila kutaja mabadiliko ya malipo ama ufadhili wa masharti nafuu.
Ilipoulizwa kutoa maelezo zaidi, wizara hiyo ilisema hakukuwa na mazungumzo kuhusu mpangilio mpya wa madeni katika mkutano huo wa Beijing.
Wizara ya fedha ya China haikujibu mara moja ombi la tamko kuhusu mazungumzo hayo.