Kenya mwenyeji wa familia ya kifalme ya Uholanzi
18 Machi 2025Ofisi ya Rais wa nchi hiyo William Ruto, imesema leo kuwa familia hiyo ya kifalme iliwasili nchini Kenya jana usiku kwa ziara ya siku tatu. Mfalme Willem-Alexander alipewa heshima ya kupigiwa mizinga 21 pamoja na kukagua gwaride la kijeshi.
Zaidi ya Wakenya 20,000 walisaini maombi kwenye tovuti ya Change.org wakiwataka Mfalme wa Uholanzi Willem-Alexander na Malkia Maxima kutafakari upya kuhusu ziara hiyo.
Soma pia: Uholanzi inataka kujiondoa katika kanuni za uhamiaji za Ulaya
Mwezi uliopita, serikali ya Uholanzi ilisema ilipokea zaidi ya barua pepe 300 zilizoomba kufutiliwa mbali kwa ziara hiyo, lakini ikasema itaendelea kama ilivyopangwa.
Siku ya Jumamosi, shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, lilizitaka Kenya na Uholanzi kuzingatia haki za binadamu wakati wa ziara hiyo.