Kenya kuwa mwenyeji wa fainali za Michuano ya CHAN
21 Juni 2025Matangazo
Akipongeza hatua hiyo, mkuu wa Shirikisho la Soka la Kenya Hussein Mohammed, aliishukuru CAF kwa imani na mwongozo wake kabla ya michezo hiyo. Mohammed ameliambia shirika la habari la AFP kwamba , macho yote sasa yameelekezwa kwa Kenya inapojiandaa kwa mashindano hayo.
Mechi za kufuzu CHAN 2025 zaendelea barani Afrika
Uwanja wa William Mkapa wa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, utakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi Agosti 2, wakati mechi ya tatu na ya nne zikichezwa katika Uwanja wa Taifa wa Mandela mjini Kampala, Uganda.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwamichuano hiyo kuandaliwa kwa pamoja na nchi tatu za Afrika mashariki. Rwanda iliwahi kuandaa michuano hiyo mwaka 2016.