Kenya kupanua mahusiano ya biashara kulinda uchumi
15 Aprili 2025Akizungumza katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola uliofanyika London, Waziri Kinyanjui alisema Kenya inalenga kupanua wigo wake wa ushirikiano wa kibiashara duniani.
Takriban nchi 25 za Afrika, ikiwemo Kenya, zimewekewa ushuru wa kulipiza kisasi katika mabadiliko ya hivi majuzi ya sera ya biashara ya Marekani, chini ya utawala wa Rais Donald Trump.Hatua hiyo ambayo utekelezaji wake umetisithswa kwa muda wa siku tisini imeelezewa na utawala huo wa Washington kuwa "tangazo la kusaka uhuru wa kiuchumi."
Mataifa ya Afrika yahimizwa kushirikiana kibiashara
Wito wake Kinyanjui unakuja wakati ambapo mataifa ya Afrika yanahimizwa kuimarishwa kwa biashara baina yao na kuendelezwa kwa viwanda vya bara hili, ili kuzuia hali ya kuuza malighafi kwa bei ya chini na baadaye kuagiza bidhaa zilizokamilika kwa gharama kubwa kutoka mataifa hayo hayo.
Kinyanjui ameongeza kusema kuwa hatua hiyo inaweza kuifanya Kenya kuimarisha uhusiano wa karibu zaidi na mataifa ya Ulaya, Asia, Mashariki ya Kati, na Amerika ya Kusini, japo Marekani na Afrika zitaendelea kuwa masoko muhimu kwa mauzo ya nguo na mavazi kutoka Kenya.
Soko kubwa zaidi la bidhaa za Kenya ni Afrika, huku Uganda ikiongoza kama mnunuzi mkuu, ikifuatiwa na Tanzania, Rwanda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hata hivyo, ushuru wa Marekani iwapo utatekelezwa unatarajiwa kuathiri sekta ya nguo na mavazi nchini, ambayo ndiyo muuzaji mkuu wa bidhaa hizo Marekani.Hata hivyo, Kinyanjui alisisitiza kuwa Kenya si miongoni mwa nchi zilizoathirika vibaya zaidi, hasa ikilinganishwa na ushindani katika soko la nguo.
Trump asema nia ya nyongeza ya ushuru ni kulinga maslahi ya Marekani
Katika kutangaza utekelezaji wa ushuru huo, Rais Trump alisema kuwa nia kuu ilikuwa kulinda maslahi ya kiuchumi ya Marekani. Hata hivyo, baadaye Trump aligeuza msimamo wake kwa kuagiza kusitishwa kwa siku 90 kwa ushuruhuo, akitaja kuwa ni kwa ajili ya mashauriano kati ya Marekani na nchi zilizoathiriwa kama Kenya. Pia alieleza kuwa nchi hizo hazikuwasilisha upinzani rasmi dhidi ya hatua hiyo.
China yatangaza ushuru kwa bidhaa za Marekani
Mkutano huo wa kila mwaka unaleta pamoja jumuiya ya wafanyabiashara wa Jumuiya ya Madola na viongozi wa serikali, mawaziri wakuu na wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Kenya ni mojawapo ya nchi zinazokua kwa kasi zaidi kiuchumindani ya Jumuiya ya Madola, ambapo zaidi ya asilimia 60 ya biashara yake ya kimataifa hufanyika na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.