Kenya huenda ikaathirika kiuchumi na sheria dhidi ya ushoga
26 Machi 2025Katika ripoti hiyo ya Open for Business kuhusu athari ya kiuchumi zitokanazo na ubaguzi kwenye eneo la Afrika Mashariki, mwenyekiti wa shirika hilo Dominic Arnall amesema sheria dhidi ya ushoga huathiri matarajio ya uwekezaji ya nchi, sifa zao kimataifa na kuzuia biashara kuvutia vipaji bora zaidi vya kimataifa.
Mapenzi ya jinsi moja ni uhalifu nchini Kenya
Tayari mapenzi ya jinsia moja ni uhalifu nchini Kenya chini ya sheria ya enzi za ukoloni, lakini sheria hiyo haitumiki sana katika nchi hiyo ambayo imekuwa kimbilio la watu wengi wanaoshiriki mapenzi ya jinsia mojakatika kanda hiyo.
Mahakama Uganda yakataa rufaa ya usajili wa kundi la LGBTQ
Lakini bado kuna unyanyapaa na ubaguzi unaozidi kuchochewa na viongozi wa kidini na wanasiasa wanaotafuta umaarufu.
Adhabu chini ya rasimu ya muswada wa kulinda familia
Rasimu ya Muswada wa Kulinda Familia imetoa wito wa adhabu kali, ikiwa ni pamoja na kifungo cha hadi miaka 50 jela kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ingawa bado haujajadiliwa bungeni.
Open for Business, imesema kuwa sheria hiyo inaweza kuongeza gharama kwa Kenya kwa kati ya dola bilioni 2.7 na 7.8 bilioni kila mwaka, kutokana na kukatizwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni na utalii, pamoja na kuongezeka kwa gharama za afyakutokana na msongo wa mawazo na utofauti wa matibabu ya virusi vya UKIMWI, miongoni mwa masuala mengine.
Mataifa kadhaa ya Afrika yamepinga waziwazi jamii zinazojihusisha na mapenzi ya jinsia moja
Benki ya Dunia ilisitisha utoaji wa mikopo kwa Uganda baada ya kupitisha Sheria ya Kupinga Ushoga ya mwaka 2023, mojawapo ya sheria kali zaidi za kupinga ushogaduniani inayobeba adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na ya kifo kwa ushoga uliokithiri.
Mataifa yapoteza ufadhili kwa ubaguzi dhidi ya mashoga
Open for Business imesema Uganda inapoteza kati ya dola milioni 586 na dola bilioni 2.4 kila mwaka kutokana na ubaguzi huo wa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Mamia ya Waislamu waandamana Kenya kupinga ushoga
Ripoti ya shirika hilo la Open for Business pia ilifanya tathmini ya nchi jirani ya Tanzania, ambayo ilisema inapoteza hadi dola bilioni 1.1 kwa mwaka, na Rwanda, yenye kiwango cha chini cha ubaguzi ikipoteza hadi dola milioni 45 kila mwaka.