Kedrman-Iran,Waokoaji waendela kutafuta watu walionusurika na zilzala.
24 Februari 2005Matangazo
Vikundi vya uokoaji nchini Iran bado vinaendelea na kazi ya kuwatafuta watu wanaoweza kuwa wamenusurika kufuatia tetemeko la ardhi lililopiga kusini-mashariki mwa jimbo la Kerman.Zaidi ya watu 500 wameuawa kufuatia zilzala hiyo ambayo ilikuwa na nguvu ya vipimo vya matetemeko 6.4 na kiasi cha watu wengine 900 wamejeruhiwa.
Mvua kubwa na theluji zimefanya kazi ya uokozi kuwa ngumu na baadhi ya wanavijiji wamekuwa wakipinga kucheleweshwa kwa misaada.
Serikali ya Iran ambayo awali ilikataa kupokea misaada kutoka nje,baadae imesema imekubali misaada hiyo,Lakini serikali ya Tehran imekataa msaada kutoka Marekani ambayo inaishinikiza nchi hiyo kuhusiana na mipango yake ya nuklia.