Guterres: Kuna ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Uislamu
15 Machi 2025Akizungumza kwa njia ya video Guterres ameitaka mitandao ya kijamii kuzuia kauli za chuki na unyanyasaji ili kukabiliana na hali hiyo. Amesema chuki hiyo inashuhudiwa huku kukiwa na ubaguzi wa watu kutokana na muonekano wao, sera zinazokiuka haki za binadamu na vurugu kwenye maeneo ya ibada.
Soma zaidi: Umoja wa Mataifa wajadili chuki dhidi ya Waislamu
Kwa miaka mingi, watetezi wa haki wameonesha wasiwasi wao kuhusu unyanyapaa unaowakabili Waislamu na Waarabu kutokana na baadhi ya watu kuzihusisha jamii hizo na makundi yenye itikadi kali za Kiislamu. Katika wiki za hivi karibuni mashirika ya kufuatilia haki za binaadamu yamechapisha taarifa zinazoonesha kiwango kikubwa cha matukio ya chuki dhidi ya waislamu katika nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Marekani na India.