Guterres asisitiza suluhisho la nchi mbili Palestina, Israel
29 Julai 2025Israel na Marekani zimetangaza kuususia. Katika ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, "njia pekee yenye uhalisia, ya haki na endelevu ni kuwa na nchi mbili- Israel na Palestina-zikiishi kwa amani na usalama, ndani ya mipaka salama inayotambulika kwa kuzingatia mipaka ya kabla ya mwaka 1967. Jerusalem ikiwa ni mji mkuu wa nchi zote na kwa kuzingatia sheria ya kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa na makubaliano mengine yanayohusika."
Mkutano huo unaendelea wakati kukiwa na ripoti kuwa Wapalestina wasiopungua 30 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Israel Ukanda wa Gaza usiku wa kuamkia Jumanne. Miongoni mwa waliouawa ni wanawake 14 na watoto 12 katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat.