KATHMANDU. Ziara ya waziri wa kigeni wa China nchini Nepal.
1 Aprili 2005Waziri wa mambo ya kigeni wa China, Li Zhaoxing, amefanya mazunguzmo na mfalme Gyanendra wa Nepal. Waziri huyo ndiye kiongozi wa kigeni wa cheo cha juu kuitembelea Nepal tangu mfalme Gyanendra alipoifuta kazi serikali na kuchukua madaraka ya kuliongoza taifa hilo miezi miwili iliyopita. Hatua yake hiyo imekosolewa na jamii ya kimataifa na India, Uingereza na Marekani zimefutilia mbali misaada ya kijeshi kwa taifa hilo. mfalme huyo alisema China ni rafiki wa kumtegemea, na mataifa hayo mawili yamefikia makubaliano kuhusu hali ya kisiasa ya Nepal. Ziara ya waziri huyo wa China imefanyika wakati waasi wa kikomunisti walipoitisha mgomo wa kitaifa kupinga hatua ya mfalme kunyakua madaraka, mgomo ambao umesababisha biashara na shule kufungwa katika maeneo ya mashariki mwa Nepal.