KATHMANDU. Maandamano ya kutaka demokrasia yafanyika nchini Nepal.
23 Mei 2005Matangazo
Maelfu ya raia wamefanya maandamano katika barabara za mji wa Kathmandu nchini Nepal, wakitaka kurejeshwa kwa demokrasia na maongozi ya kiraia katika falme hiyo ya Himalaya.
Waandamanaji kutoka vyama saba vya kisiasa, wakiwemo wabunge wa zamani na mawaziri, waliandamana kumpinga mfalme Gyanendra, aliyeifuta kazi serikali mnano tarehe mosi Februari, na kuweka vikwazo vikali chini ya sheria ya hali ya tahadhari.
Gyanendra alinyakua madaraka akisema serikali ilikuwa imeshindwa kuudhibiti upinzani wa kundi la waasi wa Mao, wanaopinga maongozi ya kifalme nchini Nepal. Machafuko ya waasi hao yamepelekea kuuwawa kwa watu wasiopungua elfu 12 tangu mwaka wa 1996.