Kasper Hjulmand: Kocha mpya Bayer Leverkusen
8 Septemba 2025Klabu ya kandanda ya Bayer Leverkusen imemtangaza kocha wa zamani wa Denmark Kasper Hjulmand kama kocha wao mpya kwa kandarasi ya miaka miwili kufuatia kutimuliwa kwa Erik ten Hag wiki iliyopita.
Hjulmand, 53, aliiongoza Denmark kutinga nusu fainali yaEuro 2020, ambapo walipoteza katika muda wa ziada dhidi ya Uingereza, na katika Euro 2024 aliishia katika hatua ya 16 bora akiwa na Denmark ambapo walitupwa nje na Ujerumani kwa kichapo cha 2-0 na baada ya hapo mwisho wake katika timu hiyo ya taifa ulifikia ukomo baada ya miaka minne.
Mdenmark huyo aliwahi kuifundisha Mainz 05 ya hapa Ujerumani msimu wa2014-15Bundesliga na sasa amerejea tena katika soka ya Ujerumani kuchukua mikoba Leverkusen.
Itakumbukwa kwamba wiki iliyopita Leverkusen ilimfuta kazi Ten Hag baada ya mechi mbili za Bundesliga. Mholanzi huyo alichukua mikoba ya Xabi Alonso ambaye kwa sasa ni kocha wa Real Madrid ya Uhispania.