KASHFA YA DIMBA UJERUMANI
3 Februari 2005KASHFA YA MARIFU WANAOCHEZESHA DIMBA UJERUMANI YAENDELEA KUGIONGA VICHWA VYA HABARI
UJERUMANI INA MIADI NA ARGENTINA JUMATANO IJAYO NA AFRIKA KUSINI NA AUSTRALIA
NA MRADI WA KIBERA WA KUWAPA MAISHA BORA WATOTO WA HALI ZA CHINI KUPITIA SPOTI
Bundesliga-Ligi ya Ujerumani ikirudwa uwanjani jumamosi hii na Bayern Munich ikiongoza kwa pointi 1 ,ni kashfa iliolikumba dimba la Ujerumani-mwaka na nusu kabla kuanza Kombe la dunia 2006- ndio inayogonga vichwa vya habari. Washtaki wa serikali wa Ujerumani,wametangaza jana kwamba, wameupanua msako na uchunguzi wao kuwajumuisha marifu watatu na wachezaji 14.
Jumla ya watu 25 wanachunguzwa kuhusika na kashfa ya kupangilia matokeo pamopja na marifu katika jumla ya mechi 10 .Kuanzia Ligi ya kwanza ya Ujerumani na ya pili-Bundesliga na ya daraja ya tatu.Pia Kombe la Shirikisho la dimba la Ujerumani,lilifanyiwa udanganyifu kama huo mwaka uliopita.
Mbali na rifu alieibua kisa hiki chote Robert Hoyzer,washtaki wa serikali wanamhoji rifu Juergen Jansen,maafisa wanaoandaa mechi Felix Zwayer na Dominik Marks.Kuungama kwa rifu Robert Hoyzer,mwezi uliopita kwamba aliopangilia matokeo ya mechi alizochezesha kulifichua kasfa kubwa kabisa ya dimba nchini Ujerumani tangu kupita miaka 30.
wachezaji 3 wa Hertha Berlin-klabu ya daraja ya kwanza ya Bundesliga waliotajwa na gazeti la FOCUS eti wamehusika na kashfa hii ya rifu na mchezo wa kamari,wamelichukulia hatua ya kisheria gazeti hilokwamba litabidi kuwalipa fidia ya Euro 250,000 likirudia mashtaka yake.FOCUS lilimtaja Muangola Nando Rafael,Josip Simunic na Alexander Madlung kuhusika na kashfa hii.
Polisi jana iliyasaka majumba watu 19 wanaotiliwa shaka na wamegundua baadhi ya ushahidi.
HUDUMA YA DRADIO DEUTSCHE WELLE KWA MASHABIKI WA KOMBE LA DUNIA 2006 NCHINI UJERUMANI:
Kombe la dunia 2006 nchini Ujerumani likijongelea na homa ya kununua tiketi za kwanza imeshawapiga mashabiki hapa Ujerumani,Radio DW kupitia mtandao wa Internet,inatoa huduma kwa mashabiki kila pembe ya dunia kuweza kujipatia taarifa kuhusu Kombe la dunia Ujerumani.Taarifa hizo zitatolewa kwa lugha mbali mbali kupitia mtandao wa Internet wa DW-WORLD.DE.
Taarifa zitatolewa kwa lugha za kiarabu,kirusi,kispain,kireno,kingereza na kijerumani.Taarifa hizo zitahusiana tangu na uuzaji tiketi,mashindano ya kuania nafasi za finali ya Kombe lijalo la Dunia, hadi wapi zinachezwa na kadhalika.
Changamoto hizo za Kombe la Dunia 2006 zilizosita wakati huu kanda mbali mbali duniani,zitaanza upya mwezi ujao wa Machi.
Isitoshe, Radio DW itawapa mashabiki matokeo ya changamoto hizo na orodha za timu za kanda mbali mbali zilipofikia katika mabara yote ulimwenguni.Na mbali na mashindano ya bahati nasibu-Quiz na Jukwaa,wenye simu za mkono-handys wataweza kujipatia taarifa juu ya timu zao kupitia mtandao wa Internet wa DW-WORLD.DE tena wakati wowote.
UJERUMANI ITACHEZA NA ARGENTINA NA AFRIKA KUSINI NA AUSTRALIA JUMATANO IJAYO:
Ujerumani ina miadi na Argentina jumatano ijayo kwa changamoto ya kirafiki.Kocha wa Ujerumani Jürgen Klinsmann ameamua kubakia nna listi yake ile ile ya wachezaji waliokwenda Asia wiki chache nyuma.Kipa wa Arsenal anaezozana na kipa mwenzake wa Ujerumani,Oliver Kahn, amechaguliwa kuwa miongoni mwa kikosi hicho.Changamoto hii mjini Düsseldorf, ni jaribio jengine la Ujerumani kutamba mbele ya Argentina tangu kupita miaka 4.
Bafana Bafana au Afrika Kusini inaikaribisha huko Durban jumatano hii ijayo Australia.Timu hizi 2 zilipokutana mara iliopita mwaka jana, Australia ilizaba Bafana Bafana bao 1:0.
Afrika Kusini ina azma pia ya kutegemea wachezaji wake wale wale isipokua mmoja tu:Imemuita mshambulizi mpya Sandile Ndlovu kuvaa jazi yao kwa mara ya kwanza.Ndlovu ndie anaeongoza pamoja na mshambulizi mwengine orodha ya watiaji magoli nchini Afrika Kusini kwa mabao yake 11.
Kocha Baxter wa Bafana Bafana ameamua kumpumzisha kipa mashuhuri Hans Vonk,lakini amewaita mastadi wake wote wanaocheza n’gambo kujiunga na timu yake.Amemuita pia stadi wa Armenia Bielefeld –klabu ya Bundesliga-Delron Buckley na hata Quinton Fortune anaeichezea Manchester United.
Katika changamoto za Ligi ya Uingereza, Chelsea juzi jumatano ilitamba tena na kuungan’gania usukani wa Premier League baada ya kuizaba Blackburn bao 1:0.Chelsea sasa iko pointi 11 kutoka Manchester na pointi 13 mbele ya mabingwa Arsenal London.
Ishara zote kwahivyo, zaonesha huu ni mwaka wa Chelsea na sio tena Arsenal au Manchester kuvaa
taji la ubingwa wa Uingereza.
Kenya kumeanzishwa mradi wa kunyanyua hali
za watoto kupitia elim u na michezo au spoti.SADILI OVAL SPORTS CLUB katika mtaa wa Kabera, kitongoji cha jiji la Nairobi,kimechaguliwa na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa kuwa shina barani Afrika la kambi za mazowezi kwa shabaha ya kuzindua tangu hisia za kimazingira hata utamaduni miongoni mwa watoto.
Kambi hizo za Shirika hilo la UNEP zinatoa kwa watoto 6,400 kutoka mtaa wa Langata,magharibi mwa Nairobi na Kabera jirani na hapo ,mtaa wa Manyata wanamoishi wanyonge n a masikini huko Kisumu pamoja na Mbaraki,mjini Mombasa fursa za mazowezi ya michezo mbali mbali na kuwa pia viongozi wa jamii zao hapo baadae.
Kituo cha Sadili pia huwafunza vijana jinsi ya kujiepusha na maradhi ya UKIMWI
na madawa ya kulevya.
Kituo hiki hivi karibuni kilimkaribisha rais wa Halmashauri Kuu ya olimpik Ulimwenguni (IOC) Jacques Chirac aliepitisha saa chache akikagua zana za kituo hicho na kutoa changamoto kwa wanafunzi wa hapo katika mchezo wa Tennis,dimba na basketball na hivyo kuwafurahisha mashabiki.
Katika shina la mradi huu mzima ni kijana wa miaka 13 Francis Isiakho.Yeye anatoka laini Saba,mtaa wa madongo-poromoka wa Kibera.Akienda shule ya Raila education Centre,lakini si kwa kawaida akihudhuria masomo.Leo hii lakini Isiakho ni mmoja kati ya mastadi kimichezo na hasa katika soka au dimba.
Akivutiwa na mwito wa kijana huyu kusaidiwa vijana katika mtaa huo wa madongo poromoka na wa kimasikini,bingwa wa zamani wa olimpik na mwenyekiti wa sasa wa halmashauri kuu ya taifa ya olimpik kip Keino,alijitolea bila ya kusita kuwasaidia vijana 2-mmojawao ni Isiakho kugharimia masomo yao ya shule ya sekondari.