Karlsruhe, Ujerumani. Matokeo ya uchaguzi huenda yasitangazwe.
14 Septemba 2005Mahakama kuu ya Ujerumani itaamua wiki hii iwapo matokeo ya uchaguzi wa bunge hapo Jumapili nchini Ujerumani yacheleweshwe kwa muda wa wiki mbili.
Kifo cha mgombea wa chama cha mrengo wa kulia mjini Dresden kimelazimisha kura katika jimbo hilo la uchaguzi kuahirishwa hadi Oktoba 2.
Msemaji wa mahakama hiyo ya katiba mjini Karlsruhe amesema kuwa maombi saba yametolewa ili kuchelewesha matokeo ya uchaguzi hapo Jumapili.
Yanadai kuwa wapigakura katika jimbo la Dresden watakuwa wanajua matokeo kabla wao kwenda kupiga kura.
Hii itakuwa na maana kwamba watapiga kura kwa mtazamo wa matokeo yaliyopo, katika uchaguzi huo ambao unatarajiwa kuwa matokeo yanaweza kulingana , na wanaweza kuwa katika nafasi ya kuamua matokeo ya mwisho.