Karlsruhe, Ujerumani. Mahakama yatoa kibali kufanyika uchaguzi.
26 Agosti 2005Mahakama kuu ya Ujerumani imesafisha njia ili kuwezesha uchaguzi mkuu kufanyika kama ulivyopangwa.
Mahakama hiyo ya kikatiba iliyoko katika mji wa Karlsruhe imeamua kuwa malalamiko dhidi ya uamuzi wa rais Horst Köhler wa kuitisha uchaguzi mwaka mmoja kabla ya muda wake, ni kinyume na sheria.
Wajumbe wawili katika serikali inayoongozwa na kansela Gerhard Schröder walipeleka malalamiko hayo.
Walidai kuwa kuitishwa kwa uchaguzi huo ni kinyume na katiba kwasababu uchaguzi huo umepangwa kufanyika kutokana na kura ya kutokuwa na imani ambayo Bwana Schröder alipanga kwa makusudi kushindwa.
Chini ya katiba hiyo , uchaguzi wa mapema unaweza tu kuitishwa iwapo kansela hatakuwa na wingi wa wabunge katika bunge la muungano , Bundestag.