KARLSRUHE: Uchaguzi wa mapema Ujerumani wapingwa mahakamani
1 Agosti 2005Matangazo
Mbunge wa Ujerumani anayepinga hatua ya rais Horst Köhler kuitisha uchaguzi wa bunge mapema, amewasilisha mashtaka katika mahakama kuu ya katiba ya Ujerumani mjini Karlsruhe.
Wasomi wa sheria wanasema jaribio hilo la kuzuia uchaguzi kufanyika mapema, lililowasilishwa na mbunge wa chama chake kansela Gerhard Schröder, cha SPD, likiungwa mkono na mbunge wa chama cha Kijani, linatarajiwa kugonga mwamba.
Mahakama ya katiba itaanza kulijadili swala hilo baadaye mwezi huu, majuma matano kabla ya uchaguzi kufanyika hapo tarehe 18 mwezi Septemba.