Karlsruhe: Mahakama ya Ujerumani yamuacha huru mtu anayedaiwa ana maingiliano na al-Qaida
19 Julai 2005Mtu aliyeshukiwa kuwa na maingiliano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida ameachiliwa huru kutoka gerezani hapa Ujerumani. Mahakama kuu ya Ujerumani imezuwia mtu huyo kupelekwa Uhispania. Polisi wa Uhispania wanataka kumfikisha mahakamani mfanya biashara huyo wa Kijerumani, mwenye asiliy a Syria, Mamoun Darkazanli, kwa mashtaka ya kutoa msaada wa fedha kwa mtandao wa kigaidi wa al-Qaida. Lakini mahakama ya Karlsruhe iliamuwa kwamba kumpeleka Mamoun Darkazanli hadi Uhispania, kupitia waranti wa Jumuiya ya Ulaya, kutakwenda kinyume na haki zake chini ya katiba ya Ujerumani. Mahakama hiyo ilisema waranti za Jumuiya ya Ulaya zinaweza tu kutekelezwa baada ya sheria mpya ya Ujerumani ipitishwe ambayo itawaruhusu mahakimu wa Ujerumani kuzichunguza amri zote za kuwasalimisha RAIA WA Kijerumani kwa nchi nyingine.