Karibu watu 65 wauawa kwenye mapigano nchini Sudan
4 Februari 2025Matangazo
Vyanzo viwili vya kitabibu, katika jimbo la Kordofan Kusini, vimesema takriban watu 40 wameuwawa na wengine 70 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi kwenye mji mkuu wa jimbo la Kadugli.
Mji huo, unaodhibitiwa na jeshi la Sudan, ulilengwa katika shambulio hilo, huku Gavana Mohamed Ibrahim akililaumu kundi la Sudan People's Liberation Movement-North (SPLM-N), linaloongozwa na Abdel Aziz al-Hilu.
Watu 65 wauawa, mapigano yakiongezeka Sudan
Mapigano makali pia yalishuhudiwa magharibi mwa Darfur, ambapo mashambulizi ya yaliulenga mji mkuu wa Darfur Kusini, na kuwauwa watu 25 na kuwajeruhi wengine 63.