Karibu watu 32 wafariki dunia kwa mafuriko Kashmir
15 Agosti 2025Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa kusimamia majanga.
Mohammed Irshad amesema timu za waokoaji zinazozunguka katika kijiji hicho cha Chositi, zimefanikiwa kuwaokoa watu 100 na kuwapeleka maeneo salama.
Irshad amesema makadirio ya awali yanaonyesha kuwa watu 50 wengine bado hawajulikani walipo.
Naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa India Jitendra Singh, amesema, mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa ya ghafla na iliyonyesha kwa muda mfupi katika kijiji hicho cha Chositi na huenda kukawa na maafa makubwa.