Karibu miili 28 yaopolewa kwenye mto Potomic, Washington
30 Januari 2025Matangazo
Ndege hiyo aina ya Bombardier CRJ ilikuwa na abiria 60 na wafanyakazi wanne pale ilipogongana na helikopta ya kijeshi wakati inakaribia kutua kwenye uwanja wa ndege Reagan Washington usiku wa kuamkia Alhamisi.
Vikosi vya uokoaji vimepiga kambi kwenye eneo la mkasa lakini hakuna matumaini ya kupatikana manusura, hali inayoifanya ajali hiyo kuwa ndiyo mbaya zaidi katika sekta ya usafiri wa anga kuwahi kutokea nchini Marekani katika kipindi cha karibu miaka 24.
Rais Donald Trump amesema amefahamishwa kuhusu mkasa huo na ametuma salamu za pole na kuwaombea wale waliopoteza maisha.