SiasaMarekani
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akosoa vikwazo dhidi ya ICC
7 Februari 2025Matangazo
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika mji wa kusini magharibi mwa Ujerumani wa Ludwigsburg, Kansela Scholz amesema ni "makosa kuiwekea vikwazo taasisi iliyo na jukumu la kuwazuia madikteta ulimwenguni kuwadhulumu watu na kuanzisha vita."
Trump alitia saini usiku wa kuamkia leo amri ya kuiwekea vikwazo mahakama ya ICC, akiituhumu kuilenga Marekani na mshirika wake mkuu, Israel.
Inafuatia uamuzi wa ICC wa kutoa hati ya kumkamata Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na kufungua uchunguzi wa madai ya uhalifu uliotendwa na wanajeshi wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza na wale wa Marekani nchini Afghanistan.