Kansela Merz kuanza ziara ya kwanza nchini Uingereza leo
17 Julai 2025Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz hii leo anaanza ziara yake ya kwanza nchini Uingereza akitarajiwa kukutana na Waziri Mkuu Keir Starmer. Viongozi hao wawili wanatarajiwa kutia saini mikataba kadhaa ya ushirikiano kama sehemu ya msukumo mpana wa kurejesha upya uhusiano wa Umoja wa Ulaya na Uingereza.
Ziara yake ya siku moja, inafanyika wiki moja baada yaziara ya siku tatu iliyofanywa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ikiashiria ushirikiano mkubwa kati ya mataifa matatu makubwa ya Ulaya, katika wakati ambao bara hilo linakabiliwa na vitisho vikubwa na kukosekana kwa uhakika na mshirka wake mkuu Marekani.
Umoja wa Ulaya unakabiliwa na mvutano wa kibiashara na Marekani tangu kurejea kwa rais Donald Trump katika Ikulu ya white House sambamba na maswali kuhusu kujitolea kwa Washington kusaidia washirika wake wa Ulaya, ikiwemo Ukraine.