Kansela Merz atilia shaka miito ya kukipiga marufuku AfD
15 Mei 2025Shirika la ujasusi la Ujerumani limekiorodhesha kuwa chama kilichothibitishwa cha msimamo mkali wa mrengo wa kulia. Merz ameliambia gazeti la kila wiki la Die Zeit kwamba lazima ithibitishwe kuwa kundi fulani linapigana kwa nguvu dhidi ya utaratibu wa demokrasia huru ya nchi kabla ya kupigwa marufuku.
Baada ya chama hicho kinachopinga sera za uhamiaji kuchukua hatua za kisheria dhidi ya hatua ya shirika la ujasusi wa ndani la Ujerumani, baadae likaubatilisha uamuzi wake hadi mahakama itakapolishughulikia pingamizi la chama hicho. Kukiorodhesha chama cha AfD kuwa kundi lililothibitishwa la msimamo mkali, ambako kunatoa mamlaka mapana kwa shirika la ujasusi kukifuatilia, kumezusha upya mjadala wa kama bunge la Ujerumani linapaswa kukipiga marufuku au la.