Kansela Merz asema vita vya Ukraine vitaendelea
27 Mei 2025Matangazo
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merzamesema vita nchini Ukraine vinatarajiwa kuendelea kutokana na kujivuta kwa Urusi kuingia kwenye mazungumzo.
Katika mkutano na waandishi habari leo, pamoja na Waziri mkuu wa Finland, Kansela Merz amesema vita humalizika ikiwa upande mmoja utaishiwa nguvu za kiuchumi au kijeshi, lakini katika suala la vita vya Ukraine bado hali hiyo haijafikiwa.
Waziri Mkuu wa Finland Petteri Orpo, amesema Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kuongeza shinikizo dhidi ya Rais Vladmir Putin kuanza mazungumzo ya kusitisha vita.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova amesema luteka za kijeshi za Finland zinageuka kuwa chombo kinachotumiwa na Jumuiya ya Kujihami yaNATOkuleta machafuko karibu na mpaka wa Urusi.