Kansela Merz aeleza wasiwasi kuhusu nafasi ya Ulaya duniani
5 Septemba 2025Matangazo
Merz ameyasema hayo wakati wa mahojiano na kituo rasmi cha habari cha chama chake CDU.TV.
Kiongozi huyo wa Ujerumani ametaja vita vya Ukraine kama mfano na kueleza kwamba Ulaya kwa sasa haina uwezo wa kumwekea shinikizo la kutosha Rais wa Urusi Vladimir Putin kuvimaliza vita hivyo.
Merz amesisitiza kuwa bara hilo linapaswa kuwa na msimamo thabiti na wa pamoja katika kulinda maslahi yake ya kiusalama, kiuchumi, na kidiplomasia
Kansela huyo ameongeza kwamba Ulaya inaitegemea sana Marekani. Licha ya wasiwasi wake, Merz amekaribisha mwanga mpya wa mshikamano wa Ulaya.