Kansela Friedrich Merz afanya ziara nchini Lithuania
22 Mei 2025Matangazo
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema usalama wa nchi washirika katika eneo la Baltic ni usalama pia wa Ujerumani.
Merz ambaye anafanya ziara nchini Lithuania nchi mshirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO, amezinduwa kikosi maalum cha kijeshi cha Ujerumani kwenye ziara hiyo.
Kikosi hicho kitakuwa na jukumu la kutoa ulinzi kwa washirika wa NATO kwenye eneo la Baltic kufuatia kuongezeka kwa wasiwasi unaosababishwa na Urusi.
Kansela huyo wa Ujerumani amesema hatua ya Berlin ya kuimarisha nguvu za jeshi lake ni enzi mpya, inayotuma ujumbe kwa washirika wake.
Rais wa Lithuania Gitanas Nauseda baada ya kukutana na Merz amesema leo ni siku ya kihistoria inayojenga hali ya kuaminiana,uwajibikaji na kufanya vitendo.