KANDAHAR Watu 14 wauwawa katika mripuko wa bomu nchini Afghanistan
1 Juni 2005Matangazo
Mripuko wa bomu umetokea kwenye msikiti katika mji wa Kandahar, kusini mwa Afghanistan. Imeripotiwa kwamba watu 14 wameuwawa katika hujuma hiyo, kati yao akiwa ni mkuu wa jeshi la polisi kutoka mji mkuu Kabul.
Wageni walisafiri kwenda Kandahar na kukusanyika katika msikiti huo kutoa rambirambi zao kwa shehe wa kiislamu aliyeuwawa kwa msimamo wake wa kuwapinga wapiganaji wa kundi la taliban. Kiongozi huyo aliuwawa Jumapili iliyopita kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa kwenye pikipiki.