KANDAHAR-mripuko wa bomu wauwa watu watano kusini mwa Afghanistan saa chache tangu Bibi Condoleeza Rice awasili nchini humo
17 Machi 2005Bomu lililotegwa kando ya barabara katika mji wa kusini wa Kandahar nchini Afghanistan limesababisha kuuawa kwa watu watano na kujeruhi wengine 32.Msemaji wa polisi nchini Afghanistan ameleekeza shutuma zake kwa kikundi cha Taleban kuwa kinahusika na mripuko huo.
Mripuko huo wa bomu umetokea saa chache baada ya kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Dokta Condoleezza Rice nchini Afghanistan,ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini humo.
Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Marekani leo alifanya mazungumzo na viongozi wa Afghanstan yaliyotuama katika kupambana na vitendo vya kigaidi na vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya.
Katika mkutano na waandishi wa habari,Bibi Rice na Rais Hamid Karzai wa Afghanistan,walitangaza kuwa nchi hiyo itafanya uchaguzi wake wa Bunge unaongojewa kwa hamu mwezi wa Septemba mwaka huu.
Marekani inaongoza vikosi vya pamoja vyenye wanajeshi 18,000 nchini Afghanistan ambao wamekuwa wakipambana na wanamgambo wa Taleban waliopinduliwa tangu mwaka 2001.