KAMPALA:Wanajeshi wa Uganda wanawatesa raia kaskazini mwa nchi hiyo.
28 Septemba 2005Matangazo
Tume ya serikali ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda,imeeleza katika ripoti yake kuwa wanajeshi wa nchi hiyo,wanawatesa raia kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo,kwa kuwafikichia pilipili machoni,kuwachoma kwa singe na kuwavuta sehemu zao za siri,ikiwa ni njia ya kuwasaka waasi wanaoendeleza vita kwa mika 19 sasa.
Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo ya haki za Binadamu ya Uganda,imeeleza katika ripoti yake iliyotolewa leo,kuwa kati ya watoto 25,000 waliokamatwa na waasi wa Lord’s Resistance Army,kiasi cha 4,000 hawajulikani walipo na huenda wamekwishauawa ama bado wapo katika kikundi cha waasi hao kama wapiganaji.