KAMPALA:Moja wa mataifa walaani kushambuliwa kwa wafanyakazi wa kutoa misaada Uganda.
27 Oktoba 2005Matangazo
Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Jan Egeland leo amelaani mfululizo wa mashambulio yaliyofanywa na waasi wa Lord’s Resistance Army(LRA) kwa wafanyakazi wa kutoa misaada katika eneo la kaskazini mwa Uganda wiki hii.
Bwana Egeland wafanyakazi wa kutoa misaada walishambulia siku ya Jumanne na Jumatano,ambapo wafanyakazi wawili waliuawa na wengine wanne walijeruhiwa.
Wafanyakazi wa vikundi vya kutoa misaada katika eneo la kaskazini mwa Uganda wamekutana leo kutathmini hali ya usalama baada ya hujuma zinazofanywa na LRA sasa kuelekezwa kwa magari yao.
Bwana Egeland amesema vitendo hivyo vya kuwashambulia wafanyakazi hao,vitasababisha kuwepo kwa hali ngumu ya maisha kwa raia wanaohitaji misaada wanaofikia milioni mbili.